Mchuano mkuu unaoleta timu bora zaidi za Kilimanjaro
Angalia Mechi za LeoTimu ya Afro Boys FC yatinga fainali na kuchukua ubingwa dhidi ya Pasua Big Stars kwenye msimu wa Tano wa Zuberi Cup Tournament
Bi Mwajuma Nasimbe amefika uwanjani kushuhudia fainali ya mashindano haya ya Zuberi Cup kwenye huu msimu wa Tano.
Msaranga FC ameshika nafasi ya Mshindi wa Tatu baada ya Kuwacharaza Kili Wonders FC kwa Bao mbili kwa Mtungi.
Uwanja wa Railway ndio uwanja mkuu unaotumika kwa mechi za muhimu za Zuberi Cup. Uwanja huu una uwezo wa kuwashika watu 1000 na umekarabatiwa hivi karibuni ili kuwa na viwango vya kimataifa. Uwanja huu ni wa khistoria na umeshashuhudia mechi nyingi za kumbukumbu.
Mabango yaliyopo kwenye uwanja mkuu wa mashindano ya Zuberi Cup yanayomuonyesha Mhe. Dkt. Samia Suluhu akiwa na Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo. Meya ni mpenda michezo na mdhamini mkuu wa mchuano wa Zuberi Cup ambao unalenga kuendeleza talanta za vijana.